Nani
SW

Letra de Nani

GéneroAfrobeats
Idioma originalSW
Vistas21
AaLectura
Tamaño 18

Letra original

SW
La traducción todavía no está disponible. Mostramos la letra original.
(Mocco) Asubuhi kumekucha Wingu limetanda Na mvua yata kunyesha Na uko mbali mama Maji takitiririka Oh baridi itanishika We ndo chanda chema Uhakika unanikatisha tamaa Utaambiwa binadamu Ah kila mmoja Ana mapungufu yake Sijui nilipoteleza mama Si ungeniambia Nimemiss tabasamu Kutwa kucha Picha kummezea mate Yangu fimbo umeibeza Ah katu hautaki kuitumia Labda hesabu za kutoa Mi niligawanya baby unisamehe Na ile hasi nikafanya chanya Baby unisamehe Na hata emoji za kulia Nazo kutumia nazo zikome Japo nipate furaha Ah huruma unionee Maana hii hali, hata haifichiki Kutwa wima cha mpingo, kisiki Maana hata nikiona michezo ya njiwa Ah huwa naitamani Kama si wewe Nitampenda nani? Nitampenda nani? Nitampenda nani Nani nitampenda Nitampenda nani? Nitampenda nani? Nitampenda nani Nani nitampenda aah Eh penzi usifanye kwa chombo cha usafiri Ikawa umeshuka uje utanikatili Nitakuwaga mental Niko dhahari Si unasikia Penzi la dhati daima la wawili We fanya na urudi lisiwe batili Ka wafanya kusudi ni ukatili Mi naumia We ndo yangu hifadhi Labda nilikosea msimbo Kweli kupenda kazi Wangu umegeuka fimbo o Mi ndo lako koroboi Lile lisilo zima Aha si ulisemaga hauchomoi Kumbe imani ulinipima ah Pia ulisema haudonoi Wameiteka mazima Ahaa simung'unyi sikohoi Sina vyangu nimechina Maana hii hali, hata haifichiki Kutwa wima cha mpingo, kisiki Maana hata nikiona michezo ya njiwa Ah huwa naitamani Kama si wewe Nitampenda nani? Nitampenda nani? Nitampenda nani Nani nitampenda Nitampenda nani? Nitampenda nani? Nitampenda nani Nani nitampenda aah

Más de Ibraah

Ibraah →

Letras relacionadas