KWETU
SW

Letra de KWETU

GéneroPop
Duración3:40
Idioma originalSW
Vistas1K
AaLectura
Tamaño 18

Letra original

SW
La traducción todavía no está disponible. Mostramos la letra original.
Sifa kwa mola wangu maulana, kwa mengi aliofanya Hadi mi na we kukutana, kisura Sijapanga kudanganya, ntasema ukweli mama Kisa nakupenda sana, kisura Umesema wanipenda, ila maisha yangu maseke Michicha, milenda ndo menyu yangu, na ya kuku mateke Yaani chenga, kila siku kilio sa lini nicheke? Sina tenda, ugali buguruni, mboga temeke Nafurahi umeniridhia niwe na wewe kimwali Maisha yangu mitihani isoisha maswali Ukifika nyumbani vumilia maana hali sio swali Asubuhi mchana pakavu, jioni ndo kula futali Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga Viwalo vyetu, ukifua kumbuka kuvilinda Huku kwetu, muda wowote mateja wanatinga Hamahm Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi Bado, mi bado, mi bado Ndo kwanza nimepanga Bado, iyee, mi bado Sina hata kiwanja Bado, iyee, mi bado Kulipa kodi majanga Bado, mimi bado, mi bado ooh ooh Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro Ghetto namkeka tu hakuna kitanda, shuka wala godoro Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya comoro Ila nimeshakupa, nimeshakupa mtima mtima Ukija kususa, utanizika mzima mzima Nimeshakupa eh, nimeshakupa mtima mtima Ukija kususa ah, utanizika mzima mzima Tena, huku kwetu muda wowote mateja wanatinga Viwalo vyetu, ukifua kumbuka kuvilinda Huku kwetu, muda wowote mateja wanatinga Hamahm Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi Bado, mi bado, mi bado (eh eh) Ndo kwanza nimepanga (eh eh) Bado, iyee, mi bado Sina hata kiwanja Bado, mie, mi bado Kulipa kodi majanga Bado, mimi bado, mi bado Suala la nyumba na gari mimi Bado, mi bado, mi bado (Haki ya mungu bado, yaani shuka bado) Ndo kwanza nimepanga Bado, iyee, mi bado Sina hata kiwanja (eh eh) Bado, iyee, mi bado (eh eh) Kulipa kodi majanga (oh uh uh) Bado, mimi bado, mi bado (iyee iyee)

Más de Rayvanny

Rayvanny →

Letras relacionadas