Atarudi
SW

Atarudi 가사

장르Pop
길이5:14
원문 언어SW
조회수3.1K
Aa읽기 설정
글자 크기 18

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
Na ye ni mwanadamu, na dunia tunapita Kama kupata kwa zamu, oh zamu, yangu itafikaa Siwezi kana damu, kesho wataja nizika Ila ningependa afahamu, haya mateso aloniipa Mmh! Tena mwambieni aloninyima mimi, ndio kampa yeye eh Kupata foleni, nasubiri yangu mimi, hata ichelewe eh Oh oh oh Sina furaha naigiza ilimradii, watoto wasijihisi vibaya Huyu mdogo anauliza eti daddy, mama ameihama kaya Cha kujibu sina nabaki tu kusema Atarudi, atarudi mama Atarudi, anawapenda sana Atarudi, atawaletea zawadi Atarudi, eh atarudi mama Atarudi, atarudi mama Atarudi, anawapenda sana Atarudi, atawaletea zawadi Atarudi Siwezi sema sijui tatizo, hali yangu duni imefanya ukanikimbia Ni vyema ungefanya maigizo, mara kumi usingenizalia Mmmh, ingali mapenzi pekee, ningesema ni changamoto nijifunze Ameniacha mpweke, na watoto niwatunze Eh, ila siwezi laumu (ah), wenda yupo sawa (ah) Kipato changu kigumu (ah), kutwa bumunda na kahawa (ah) Eh! Ila mwambieni aloninyima mimi, ndio kampa yeye eh Kupata foleni, nasubiri yangu mimi, hata ichelewe Oh oh oh Sina furaha naigiza ilimradi, watoto wasijihisi vibaya Huyu mdogo anauliza eti daddy, mama ameihama kaya Cha kujibu sina nabaki tu kusema Atarudi, atarudi mama Atarudi, anawapenda sana Atarudi, atawaletea zawadi Atarudi, eh atarudi mama Atarudi, atarudi mama Atarudi, anawapenda sana Atarudi, atawaletea zawadi Atarudi

Harmonize의 다른 곡

Harmonize →

관련 가사