Mapenzi
SW

Mapenzi 가사

장르Regional
원문 언어SW
조회수11
Aa읽기 설정
글자 크기 18

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
Kama ni mapenzi Ya kuniudhi kila saa Ya kunifanya mi kulia Na kama huridhiki Na mbona hujasema Ili niweze rekebisha Nifanye mambo shwari Nikiamini u kwangu Na kukusifu kwa wazazi Hujali tenda hisia zangu Sijui tunapokwenda Lakini najua tulipotoka Kutoka sitoki nimetekwa nyara Kukuwacha siwezi kibarua ngumu Nashindwa ni nini ntafanya uridhike Nimetekwa ndani Mtandao wa mapenzi Basi nakuomba Uniteke tu bila mateso Tazama, nimezama Ndani ya bahari La penzi lako Siwezi Kusonga mbele Kurudi nyuma Sijielewi Haya mapenzi ya fujo hayafai Kama wanipenda Jaribu kunipa raha Mi nashangaa Watu wakisema Eti tunapendana Japo tunazozana Ni vizuri mami Nyumba kuwa na siri Lakini jaribu Tusuluhishe Bila hivyo Itakuwa mchezo Wa kuigiza Kwenye mambo bandia Mimi sitaki Mambo ya kujifanya Ati tunapendana Tena tunatesana Nimejaribu sana kujitoa ndani Kila nikipanga napangua mwenyewe Natamani sana ungeelewa hivyo Mimi mateka Mimi pumbavu Wa penzi lako Nieleze ni lini ntakuwa huru Tazama, nimezama Ndani ya bahari La penzi lako Siwezi Kusonga mbele Kurudi nyuma Sijielewi Haya mapenzi ya fujo hayafai Kama wanipenda Jaribu kunipa raha Jaribu baby Mambo Ya kunifanya kumbafu haifai Mambo yo yo yo yo yo Haifai Jaribu baby Tusuluhishe Nimejaribu sana kujitoa ndani Kila nikipanga napangua mwenyewe Natamani sana ungeelewa hivyo Mimi mateka Mahabusu Wa penzi lako Nieleze ni lini ntakuwa huru Tazama, nimezama Ndani ya bahari La penzi lako Siwezi Kusonga mbele Kurudi nyuma Sijielewi Haya mapenzi ya fujo hayafai Kama unanipenda Jaribu kunipa raha

관련 가사