Shida
SW

Shida 가사

장르Pop
원문 언어SW
조회수48
Aa읽기 설정
글자 크기 18

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
Natoka zangu kwetu kibiti Naisaka dar es salaam Naenda tafuta riziki Niwatunze baba na mama Nikizunga haba na haba Ndio kilo inatosha Chunga miguu kuvaa rubber bana Zisizo kutosha Anayesema riziki mafungu saba Anakupotosha Riziki mafungu mawili Kupata au kukosa Aliyoyasema baba Heshima ya nyumba si dirisha Dunia ni saa mbovu mwana Usije ifwatisha Vingine vinakaba Lazima unywe maji kupitisha Umia upate kovu baba Maumivu yatakwisha Hata mate kinywani ya uchungu Nayameza kwa tabu jama Maisha yangu mazingaombwe Ya maajabu sana Oooh mama oooh Eeeeh mama eeeh Ooooh shida ooooh shida Ooooh shida ooooh shida Shida zitakwisha lini Ooooh shida ooooh shida Ooooh shida ooooh shida Shida zitakwisha lini Najipa matumaini Nitafute nisichoke Moyoni nikiamini kuwa Mungu ni wetu sote Ila mbona kwangu sasambu sasambu Sipati usiku si mchana Ama kitabu cha riziki yangu Tayari kimechanwa Eeeeh eh eeeeh Baba mama chama na mogela Yani mimi ndio nategemewa Nakaza nashinda kombolela Likipigwa nabutua hewa Hata mate kinywani ya uchungu Nayameza kwa tabu jama Maisha yangu mazingaombwe Ya maajabu sana Oooh mama oooh (oooh) Eeeeh mama eeeh (oh oooh) Ooooh shida (ooooh shida) Ooooh shida (ooooh) Ooooh shida Shida zitakwisha lini (mama mama eeh) Ooooh shida (mama mama eeh) Ooooh shida (mama mama aaah) Ooooh shida (ooooh) Shida zitakwisha lini

Mbosso의 다른 곡

Mbosso →

관련 가사