Ibaki Story
SW

Ibaki Story 가사

장르Pop
원문 언어SW
조회수22
Aa읽기 설정
글자 크기 18

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
Matapishi ni kinyaa kuzirudisha tena kwenye kinywa Japo mengi ulisema, kama nuru ghafla ukazima Ikawa ngumu kukusahau, nikasema moyo ukome Kwa kali sulu na madharau, penzi ulivunja na ngome Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Kiliniumiza kitanda na shuka tuliolalia Mapenzi yana siri kubwa, sishangai mtu akilia Nimekubali mboni zangu zimtazame mwingine Maridhia ya moyo wangu huenda si fungu pengine Cha kushangaza hadharani mengi ya kuficha ukaweka wazi Nikahisi sijui mapenzi, labda kwako sinogi nazi Na unajua hata nikilia, siwezi kutokwa na machozi We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Yalinitesa mazoea aya Lakini mi nishazoea mwaya Ila tambua mapenzi mabaya Kidonda chake hakinaga dawa Ee mazoea aah Lakini mi nishazoea mwaya Ila tambua mapenzi mabaya Kidonda chake hakinaga dawa Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, uuh, uuh Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, uuh, uuh

관련 가사