Faraja
SW

Faraja 가사

장르Pop
원문 언어SW
조회수14
Aa읽기 설정
글자 크기 18

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
Faraja nakutafuta hauonekani? Mawazo yananitinga moyo unauma faraja ooh! Uniondoe upwekee, usiniache peke Dunia imenitupa ndungu wamenitupa ooh! Pesa hakuna, chakula hakuna Matatizo makubwa, upweke umenikumba Pesa hakuna, chakula hakuna Matatizo makubwa, upweke, upweke, upweke eeh! Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja ooh! Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh! Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja Dunia inanichanganya, natafuta faraja ooh! Wapo wengi sana, wakuhitaji faraja Unikumbuke sana, nami ni wa mmoja Ukifika kwangu, ukae mwaka mmoja Tutembee pamoja, nitambe nawe faraja Lakini ukija leo na uondoke keshoo Utaniachia mawazo kichwani tele mawazo Pindi mimi sina pesa, wengine wanatesa Ninapokua nawaza uwa uwa nakuhitaji faraja ooh! Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja ooh! Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh! Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja Dunia inanichanganya, natafuta faraja ooh! Nimezalishwa mwana, baba sijamuona Nyumba niliyopanga karibu ninafukuzwa Nimeshauza nyanya, maandazi hata karanga Faida sikupata, sasa nafa na njaa Ona barabarani wanavyo omba omba Nenda kwao faraja, wanakuita faraja Alau uje sasa ukae nami faraja Mpaka lini mola maisha haya mabaya ooh! Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja ooh! Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh! Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja Dunia inanichanganya, natafuta faraja ooh!

Lady Jaydee의 다른 곡

Lady Jaydee →

관련 가사